20 Julai 2019 - 07:45
Kusimamishwa meli ya kigeni katika Ghuba ya Uajemi; mapambano ya Iran dhidi ya magendo ya mafuta

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC au SEPAH limetangaza kwamba limetumia kibali cha mahakama kusimamisha meli moja iliyokuwa imebeba mafuta ya magendo katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

(ABNA24.com) Jeshi hilo jana Alhamisi baada ya kuhakikisha kwamba meli moja ya kigeni ilikuwa imebeba lita milioni moja za mafuta ya magendo, na kupata kibali kutoka kwa maafisa husika wa vyombo vya mahakama vya humu nchini, lililazimika kuisimamisha meli hiyo kusini mwa Kisiwa cha Larak katika Ghuba ya Uajemi. Hatua hiyo ya SEPAH imetekelezwa katika fremu ya majukumu yake mazito ya kulinda usalama katika maji ya Ghuba ya Ujemi na Lango Bahari la Hormoz. Jukumu kuu la jeshi hilo la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo hilo, ni kulinda maslahi ya taifa la Iran, usalama na kupambana na magendo ya baharini. Kwa mujibu wa Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jeshi hilo, ikiwa ni katika kutekeleza jukumu lake la kupambana na magendo ya mafuta, kila siku huchukua hatua kama vile za kusimamisha meli zinazobeba mafuta ya magendo katika Ghuba ya Uajemi.

Eneo la Ghuba ya Uajemi na hasa Lango Bahari la Hormoz, lina nafasi muhimu katika uchumi wa dunia, hivyo jukumu la Jeshi la Walinzi wa Mapindfuzi ya Kiislamu katika kulinda usalama wa eneo hilo lina umuhimu wa kistratijia.

Katika uwanja huo, Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema jana kwamba eneo la Ghuba ya Uajemi, Lango Bahari la Hormoz na visiwa vinavyolizunguka  ni eneo nyeti, muhimu na lisilotenganishika na uchumi wa dunia, si kwa Iran pekee, bali kwa ulimwengu mzima.

Kwa kutilia maanani umuhimu wa kimataifa wa Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz, Iran ina jukumu muhimu la kulinda usalama wa eneo hilo kwa shabaha ya kudhamini mahitaji ya nishati ya ulimwengu.

Kusimamishwa kwa meli iliyotajwa ya kigeni iliyokuwa imebeba mafuta ya magendo na Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kunaonyesha nafasi chanya ya Iran ambayo inadhibiti kikamilifu matukio ya baharini na kukabiliana vilivyo na tukio lolote linaloweza kuvuruga mkondo wa kudhaminiwa nishati katika masoko ya dunia.

Licha ya kuwa magendo ya mafuta yanahatarisha maslahi ya taifa la Iran pia yanachukuliwa kuwa ni changamoto muhimu ya kimataifa. Kitenfo cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha kusimamisha meli hiyo ya kigeni iliyokuwa imebeba mafuta ya mgendo licha ya kuwa ni utekelezaji wa jeshi hilo wa majukumu yake ya kitaifa pia ni alama ya uwajibikaji wake katika kulinda usalama wa mkondo wa kudhamini nishati ya kimataifa. Hatua hiyo imetekelezwa kikamilifu katika fremu ya sheria za ndani ya nchi na vilevile za kimataifa kuhusiana na masuala ya ubaharia na safari za baharini.

Jeshi hilo limechukua hatua hiyo baada ya kupitia hatua zote za kisheria na kupata kibali kinachohitajika kwa ajili ya kusimamisha meli hiyo iliyokuwa imebeba mafuta ya magendo. Sheria za ubaharia zinasema kuwa meli yoyote isiyo ya kijeshi au isiyo ya serikali inayovunja sheria za ubaharia, ukiwemo uharamia, ulanguzi wa madawa ya kulevya, kutangaza vipindi vya redio au televisheni visivyoruhusiwa na kukataa kupeperusha bendera ya utambulisho, inaweza kusimamishwa na kukaguliwa.

Kwa kutilia maanani kwamba kitendo cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha kusimamisha meli hiyo iliyokuwa imebeba mafuta ya megendo kina msingi wa sheria za ndani na nje ya nchi, radiamali hasi ya Marekani na kukosoa kwake hatua ya Iran kuhusiana na suala hilo, inathibitisha wazi mtazamo wa kisiasa wa Washishington juu ya suala hilo na uungaji mkono wake kwa vitendo vya ulanguzi na magendo ya mafuta katika Ghuba ya Uajemi.



/129